habari Mpya


Sare Feki za Jeshi Zakamatwa Kambi ya Wakimbizi Kibondo.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma, imekamata nguo zinazofanana za sare za Jeshi katika Kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli pamoja na Nduta.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari, January 10, 2019, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma SAMSON ANGA, amesema nguo hizo zilikamatwa December 31, 2018 ,Jumla ni 1,947 huku katika Kambi ya Mtendeli zikikamatwa nguo 622 na Nduta ni 1,325 uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini walioingiza sare hizo na lengo lao.

MSIKILIZE HAPA CHINI-BOFYA PLAY
Source-Millardayo

Post a Comment

0 Comments