habari Mpya


Naibu Waziri Aweso Aagiza Mhandisi wa Maji Muleba Akamatwe.

Na Shafiru Yusuf –RK Muleba.

Naibu Waziri wa Maji wa Tanzania, Bw Juma Aweso ameagiza Jeshi la Polisi Wilayani Muleba Mkoani Kagera kumkamata Mhandisi wa Maji wilaya ya Muleba Bw. Bonifas Rukoho baada ya kuwepo mapungufu mbalimbali kwenye mradi wa maji wa Katoke.

Bw. Aweso ametoa maagizo hayo baada ya wananchi wa kata hiyo

kulalamikia mradi huo ambao umeanza kujengwa tangu mwaka 2013 hadi sasa hautoi maji.
Amesema Jeshi la polisi limkamate mhandisi wa wilaya hiyo kwa ajili ya mahojiano zaidi juu ya mradi huo.
BOFYA KITUFE CHA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA ZAIDI.

Awali akisoma taarifa mbele ya Naibu Waziri, Mhandisi wa Maji wa wilaya hiyo Bw. Bonifas Rukoho amesema mradi huo ulitarajia kugharimu zaidi ya shilingi milioni 476 lakini kwa sasa mkandarasi ameishalipwa jumla ya shilingi milioni 404 na tayari ameshaukabidhi.

Post a Comment

0 Comments