habari Mpya


Haruna Niyonzima Aipeleka Simba SC Nusu Fainali Mapinduzi Cup 2019.

Simba SC wameibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mlandege FC kwenye mechi yake ya mwisho ya Makundi ya Kombe la Mapinduzi Cup 2019.

Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 9 baada ya kucheza mechi tatu na kuendelea kuongoza Kundi A.

Bao pekee la Simba SC katika mchezo huo lilifungwa na kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima dakika ya 21  kwa penalti iliyotolewa na refa Rashid Farhan baada ya beki Asante Kwasi wa Simba SC kudondoshwa kwenye ndani boksi.

Baada ya kuwa kinara wa Kundi B , Simba SC watacheza mechi ya nusu fainali dhidi ya timu iliyomaliza nafasi ya pili Kundi A, ambapo Simba SC sasa kwa michezo iliyobakia italeta Team B imalizie michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments