habari Mpya


DC NGARA...."Tutawafungia wafanyabiashara wadogo ambao hawatachukua vitambulisho".

Na Auleria Gabriel, Ngara. 
Uchukuaji wa vitambulisho vilivyotolewa na rais Dakt. John Magufuli kwa wajasiriamali wadogo umeonekana kukwama wilayani Ngara mkoani Kagera kutokana na mwitikio mdogo wa wajasiriamali hao kujitokeza kuchukua vitambulisho

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanal Michael Mtenjele, amesema wilaya ilipokea vitambulisho elfu 3570 lakini mpaka sasa vimeshatolewa vitambulisho 577 pekee.

Kufuatia hali hiyo, Mtenjele ametoa onyo kwa wajasiriamali wenye vigezo ambao hawajachukua vitambulisho wafanye jitihada za kuvipata kabla hatua zaidi hazijachukuliwa kwakuwa anakuwa anaiibia serikali.

Naye kaimu afisa biashara wa wilaya ya Ngara Bi. Adelina Mapunda amesema zaidi ya wafanya biashara elfu tatu hawapo katika mfumo rasmi wa malipo hivyo wameanza kupita kwa kila kata ili kutoa elimu zaidi juu ya umuhimu wa vitambulisho hivyo.

Post a Comment

0 Comments