habari Mpya


DC Kasulu Akabidhi Vitabu 500 Vya Stakabadhi Kwa Watendaji wa Kata kwa Ajili ya Ujenzi wa Madarasa.

Mfano wa Stakabadhi/Receipt.

Na Philmon Golkanus –RK Kasulu 94.2.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kanali Simon Anange amekabidhi vitabu 500 vya stakabadhi kwa watendaji wa kata za halamashauri ya mji wa Kasulu kwa ajili ya michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Akikabidhi vitabu hivyo Kanali Anange amewataka watendaji kuwa waadilifu wakati wa zoezi la ukusanyaji michango na kwamba atakayekiuka na kuonesha udanganyifu hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha mkurugenzi wa halmashauriya mji wa Kasulu Bi. Fatna Laay amesema kupitia vitabu hivyo wanataraji kukusanya shilingi Milioni 200 zitakazotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuwezesha wanafunzi kupata nafasi ya masomo mwaka 2019.

Hivi karibuni kupitia mkutano uliowakutanisha wananchi, viongozi na wadau wa elimu wa halamashauri ya mji wa Kasulu, walijadiliana namna ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo.

 Wanafunzi elfu 1 na 845 wako katika hatari ya kukosa nafasi ya Masomo ya Sekondari.

Post a Comment

0 Comments