habari Mpya


Ajali ya Basi yaua Watu Wanne na Kujeruhi 42 Kigoma.

Basi la kampuni ya FIKOSHI likiwa limeharibika baada ya ajali.

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 42 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya FIKOSHI linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Mwanza kupoteza mwelekeo na kupinduka katika eneo la Uvinza mkoani Kigoma usiku wa kuamkia leo January 24, 2019.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma MARTIN OTIENO, amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva wa basi hilo, na kusababisha kupinduka.

Amesema Ajali imetokea maeneo ya Uvinza, kuna sehemu inaitwa Mnarani, ni barabara ya Vumbi, ilipofika maeno hayo ambayo ina kona kona nyingi, kwa mujibu wa mashuhuda wamesema dereva alikuwa kwenye mwendo kasi, alipofika maeno hayo, gari ikapinduka na kusababisha vifo vyo watu wanne wanaume watatu na mwanamke mmoja huku majeruhi 42.

Kamanda Otieno amesema Majeruhi  wanapatiwa matibabu katika  hospitali ya Maweni ya Mkoa wa Kigoma.

Post a Comment

0 Comments