habari Mpya


Walichokisema Rais Dkt. Magufuli, Mhe. Job Ndugai na Mbunge John Mnyika Wakati wa Uwekaji Jiwe la Msingi Upanuzi wa Barabara Kimara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya mradi wakati wa hafla  ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .


Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19,2018Ni Sauti ya Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai aikizungumza jumatano december 19,2018  katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara  wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara hadi Mbezi jijini Dar es Salaamna hafla hiyo  imefanyika   neo la Kimara Stop Over.Ni Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), John Mnyika amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuweza kuamua kujenga barabara ya njia nane  lakini pia amemuomba kukumbuka malalamiko ya wananchi wa eneo hilo waliobomolewa nyumba zao wakati wa ujenzi wa barabara.Rais Magufuli akizungumza  katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara  ya Morogoro eneo la Kimara hadi Mbezi jijini Dar es Salaamna hafla hiyo  imefanyika   eneo la Kimara Stop Over ambapo amesema waliobomolewa nyumba kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara hadi Mbezi jijini Dar es Salaam hawatalipwa fidia kwa kuwa walijenga katika eneo la hifadhi ya barabara.

Post a Comment

0 Comments