habari Mpya


Wakulima wa Zao La Pamba Sengerema Waache Kilimo Cha Mazoea.

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Nyampande wakizungumza na Radio Kwizera wakati wa uzinduzi wa msimu mpya  wa Pamba wamesema kuwa wanataraji kupata mafanikio mazuri kutokana na kwamba Serikali inahamasisha upandaji wa kisasa ambao tayari unatekelezwa.


Na Erick Ezekiel –RK Sengerema 97.7.
Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri ya Sengerema Mkoani Mwanza Bw.Simon Butera.

Wakulima wa Zao la PAMBA wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa   kuzingatia   upandaji bora wa mbegu za zao hilo kulingana na maelekezo ya kitaalamu ili kupata mazao bora na kuepuka pamba kuharibika bila kukomaa.

Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Sengerema Bw.Saimoni  Butera ameiambia Radio Kwizera kuwa mpaka kufikia sasa jumla tani 135 za mbegu zimekwisha pokelewa na idara yake  ambazo tayari zimewafikia wakulima kwa ajili ya kuanza upandaji.

BOFYA PLAY KUSIKILIZA NAMNA BORA YA KULIMA KITAALAM ILI KUPATA MAVUNO MENGI YA PAMBA.

Post a Comment

0 Comments