habari Mpya


Ubovu wa Barabara ya Lusahunga hadi Ngara mkoani Kagera na Fursa kwa Vijana.

Na Shaaban Ndyamukama-  RK Biharamulo 97.9.

Muonekano wa baadhi ya watoto  walioamua kujitolea kuisaidia Serikali kukarabati barabara iliyojaa mashimo inayotokea eneo la Lusahunga wilayani Biharamulo hadi wilayani Ngara mkoani Kagera,na kuchakaa kwa barabara hiyo imekua chanzo cha ajali zikisababisha uharibifu wa mali,magari , watu kufariki na wengine kujeruhiwa.

Watoto hao ni wenye umri wa kwenda shule  wanaosoma darasa la tatu hadi la sita  shule ya msingi Nyamalagala na hutumia majembe ya mkono  kuchimba udongo   kuziba mashimo.
Kijana Amos Gervas (13) anasema  ukarabati wa barabara hufanyika siku za jumamosi na jumapili na wakati huu wa likizo huku madereva wengine hutulipa Shilingi 200 hadi Shilingi 500  na tunazikusanya kwa siku tunagawana na kwenda kununua sabuni za kuogea na kufulia pamoja na kupata madaftari au kalamu kwa matumizi ya shuleni.
Madereva,Abiria na Wananchi wa kawaida wanaotumia  barabara hiyo wamesema wanapata wakati mugumu wa kusafirisha bidhaa zao kwenda mikoani kwa ajili ya kuuza hasa ndizi , alizeti na mihogo mikavu pamoja na matunda ya aina mbalimbali.

Helman John mkazi wa Nyakahura mzani wilayani Biharamulo amesema maereva wanakaa kwenye barabara hiyo kwa siku nyingi baada ya vyuma vya magari kukatika na kuwa omba omba wa chakula wakisubiria vipuli vipya.

Naye  Afisa Msaidizi wa TRA kituo cha Forodha Kabanga wilayani Ngara Seifu Mkilindi anasema magari yanayopita kituoni hapo yakitokea barabara ya Lusahunga  kwa siku ni kati ya 80 hadi 100 yenye mizigo kuanzia tani 1 hadi 30 kwa siku moja.

Pia Afisa Mfawidhi wa kituo cha Forodha Rusumo Policarp Bashaho  alisema magari yanayopita eneo hilo yenye mizigo kwa tani 30 ni kati ya 170  na magari madogo ya tani moja (IT) ni wastani wa magari 20 kwa siku moja.

Naibu wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi  Mhe.Elias  Kwandikwa  ameahidi  barabara hiyo  kutengenezwa yenye urefu wa kilomita 91 iliyojengwa miaka 34 iliyopita  baada ya kupatikana fedha toka benki ya Maendeleo ya Afrika pia benki ya dunia.

Amesema pia fedha nyingine zitatoka Benki ya dunia kwa kuungana na bajeti ya fedha za mapato ya ndani   baada ya kuanza ujenzi wa kilomita 15 kutoka Nyakanazi hadi Lusaunga kupitia Kampuni ya  Stanbarberg  ya nchini ujerumani.

Post a Comment

0 Comments