habari Mpya


Simba na Mtibwa Sugar wafanya Vyema Mashindano ya CAF.

Mabingwa Tanzania,Timu ya Simba, imeibuka na ushindi  wa bao 4-0 dhidi  ya Mbambane Swallows ya Swaziland katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa leo December 4,2018  mjini Mbabane. 

 Kwa ushindi huo, Simba wamewatupa nje ya mashindano hayo  Mbambane Swallows kwa jumla ya mabao 8-1. Mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda mabao 4-1.
Wafungaji wa Simba katika mechi hiyo ni  Cletus Chama dakika 28 na 33, Emmanuel Okwi  dakika 51 na Meddie Kagere  dakika ya 63.
Nacho Kikosi cha Mtibwa Sugar, kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Northern Dynamo katika mchezo wa marudio wa kombe la shirikisho Afrika uliochezwa katika visiwa vya Shelisheli.

Bao la Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 68 bada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Chamazi, Mtibwa walifanikiwa kushinda kwa mabao 4-0 hivyo mzigo waliokuwa nao Dynamo leo ulikuwa mzito kuweza kufunga mabao 5-0.

Kwa matokeo hayo Mtibwa wanafanikiwa kusonga mbele katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wa leo ugenini.

Post a Comment

0 Comments