habari Mpya


Sheikh Zakaria Kagimbo: Wauguzi Toeni Huduma Bora kwa Wagonjwa .

Na Shafiru Yusuf –RK Muleba.

Baraza Kuu la Waislamu wilaya ya Muleba Mkoani Kagera  limetembelea kituo cha Afya Kaigara na kuwaombea dua wagonjwa pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali.

Akiongoza Msafara wa Waislamu Sheikh wa wilaya ya Muleba Sheikh Zakaria Kagimbo amewataka watoa huduma ya afya katika kituo hicho kufanya kazi kwa weledi mkubwa na kuwa na kauli nzuri kwa wagonjwa.

Amesema kuwa kauli nzuri inamfanya mgonjwa kuwa na matumaini ya kupoma, hivyo ni wajibu wa kila mtumishi wa kituo hicho cha afya kuwa na mahusiano mazuri na wagonjwa na waweze kupona haraka.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kaigara Bw. Alibert Bongo amesema kuwa kituo hicho kina upungufu wa nyumba za Watumishi hali inayopelekea wagonjwa kushindwa kupata huduma kwa wakati kutokana na wengi wa watumishi kukaa nje ya kituo hicho.

Post a Comment

0 Comments