habari Mpya


Mugoma Shule ya Msingi –Bingwa wilaya ya Ngara Bonanza la Michezo ya Jambo Bukoba.

Mabingwa wa Bonanza Mugoma shule ya Msingi (pichani),wilayani Ngara mkoani Kagera sasa kuiwakilisha wilaya katika Bonanza la Michezo ya Jambo Bukoba kimkoa January 2019 wakiibuka na ushindi wa 80% wakifatiwa na mshindi wa pili Lemela na 76% wa tatu Murutabo 64% wa nne Kirusha 61% wa tano Shanga 61%huku wa sita ni Katerere 60%...na Jambo Bukoba inaadhimisha miaka 10, sasa mshindi wa kwanza na wa pili kwa kila Bonanza atazawadiwa shilingi milioni 4.
Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kupitia Idara ya Elimu shule za Msingi Jana November 30,2018 imeendesha Bonanza la michezo ya Jambo Bukoba la siku moja huku Bonanza hilo likifadhiliwa na shirika la Jambo Bukoba la mkoani Kagera ili kupata timu Moja Bingwa itakayoiwakilisha wilaya ya Ngara katika Bonanza la michezo hiyo la Mkoa mwezi January 2019.


Jumla ya Shule 6 za msingi zilizofuzu nafasi ya kushiriki Bonanza hilo ,zimeshindana kwa kucheza michezo ya aina nne kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mugoma.
Steven Gonzaga–ni Meneja Michezo, Shirika la Jambo Bukoba mkoani Kagera anasema Bonanza la Mkoa ambalo litafanyika January 2019, katika Manispaa ya Bukoba –litatumika pia kuadhimiasha miaka 10 ya uwepo wa shirika hilo la Jambo bukoba ambalo limekua likijihusisha kuwajengea walimu wa michezo mbinu za kuwafundisha wanafunzi wa shule za msingi michezo mbalimbali na Kuibua vipaji pamoja na Kuviendeleza

MSIKILIZE HAPA.

Post a Comment

0 Comments