habari Mpya


Mtoa Burudani Siku ya UKIMWI Katika Viwanja Vya Posta ya Zamani Mjini Ngara.

Picha Na Shaban Ndyamukama –RK Ngara.

Mtoa Burudani katika pozi  la kusherehesha Katika Viwanja Vya Posta ya Zamani Mjini Ngara mkoani Kagera wakati wa Siku ya Ukimwi Duniani iliyoadhimisha Kimkoa leo December 1, 2018 ambayo huadhimishwa kila tarehe 1 December kama siku maalumu ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa wa UKIMWI.

 Desemba mosi ilichaguliwa kuwa siku ya Ukimwi kutokana na tarehe hiyo kuwa ndiyo siku ambayo virusi cha Ukimwi kilitambulika rasmi mwaka 1981. 

Haya ni maadhimisho ya 30. 

Shirika la afya duniani WHO linasema, watu Milioni 37 duniani, wanaishi na maambukizi ya ukimwi huku vijana wakiendelea kuwa hatarini zaidi kuambukizwa hasa barani Afrika.

Watu wengine Milioni 22 walioambukizwa, wanatumia dawa ya AVR ambayo imesaidia watu wengi sana kuendelea kuishi.
Siku hiyo ilichaguliwa rasmi mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa Dunia wa Mawaziri wa Afya Kuhusu Mpango wa Kuzuia Ukimwi. 

Kuanzia hapo siku hiyo imekuwa ikikumbukwa rasmi na SERIKALI, MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI, NA WANAHARAKATI
, kutoa elimu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, kupiga vita unyanyapaa na kuhimiza watu kwenda kufanya vipimo ili kufahamu hali zao.

Woga, unyanyapaa na kupuuza ni mambo ambayo yanaendelea kuitesa dunia katika mapambano ya ugonjwa huu ambao umesababisha vifo vya Mamilioni ya watu tangu miaka 1980.

Maambukizi mapya yanawaathiri idadi kubwa ya vijana walio na umri wa kati ya miaka 15-25. Katika vijana watano, watatu ni vijana wa kike.

Uchunguzi wa WHO umebaini kuwa, asilimia 71 ya maambukizi mapya yanatokea barani Afrika, hasa eneo la Afrika Mashariki na Kusini mwa bara hilo.

Kila mwaka siku hiyo hufanyika kwa ujumbe maalumu. Ujumbe wa mwaka 2018 ni, " kufahamu hali yako, ni muhimu kwa kupima.". 
 

Post a Comment

0 Comments