habari Mpya


Mkazi wa Kasulu Usiyekuwa na Choo, Unakabiliwa na Kifungo, Faini au Vyote kwa Pamoja.

Hiki choo kimekosa sifa 3 kua choo bora

  •  Hakina paa
  • Hakina mlango
  •  Hakina bomba la kutolea hewa

Na Albert Kavano-RK Kasulu 94.2.


Serikali wilayani Kasulu mkoani Kigoma imesema wananchi watakao kuwa hawana vyoo Nyumbani na nyumba za Biashara ndani ya siku saba baada ya kupewa notisi wanakabiliwa na Kifungo, faini au Vyote kwa pamoja.


Amri hiyo imetolewa leo December 6,2018 na Mkuu wa wilaya ya Kasulu KANAL SIMON ANNANGE wakati akiongoza Kampeni ya kuboresha na ujenzi wa vyoo bora ndani ya halmashauri za mji na wilaya ya Kasulu.
 
Kanal Annange amesema anatekeleza Agizo la waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo anayewataka wananchi nchi nzima kuwa na Vyoo bora ifikapo Disemba 31 mwaka huu,2018 na watakao kiuka maagizo hayo adhabu yao  ni Faini isiyopungua shilingi milioni moja, Kifungo cha mwaka mmoja gerezani au vyote kwa pamoja.

PLAY KUMSIKILIZA DC KASULU.

Kwa upande wake,Afisa Afya Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw. Nimrod Kiporoza amesema wameanza kutembelea mitaa na vijiji vyote wilayani humo , kutoa notisi ya siku saba za mpito ambapo zikiisha sheria itafuata mkondo wake.

Post a Comment

0 Comments