habari Mpya


Kagera Yapunguza Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

KAGERA NA SHAABAN NDYAMUKAMA.
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika halmashauri nane za mkoa wa Kagera yametajwa kupungua lakini  changamoto iliyobainishwa na wahamasishaji ni wanaume kutojitokeza kupima afya zao kwa hiari katika kampeni zinazoendelea.

 Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia jenerali Marco Gaguti amebainisha hayo jana kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani katika taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni kanali Michael Mntenjele.
Taarifa ya mkoa wa Kagera imeeleza kuwa Wilaya ya Misenyi  inayo Maambukizi ya asilimia 1.8, Ngara  asilimia 0.5, Muleba asilimia1.7 , Biharamulo asilimia1.0 Bukoba vijijini asilimia 1.7  Bukoba manispaa asilimia1.7 hivyo jamii kutakiwa kuwa na uaminifu katika  ndoa zao.


Januari hadi Oktoba mwaka huu mkoani Kagera waliojitokeza kupima afya zao walikuwa 1,2 91,735 kati yao  watu 16,048 walikutwa na maambukizi sawa na asilimia 1.2 kwa mkoa wa Kagera ambapo maambukizi yamepungua kutoka asilimia 1.6 kwa mwaka 2017.
Naibu katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Amon Mpanju ameitaka jamii ya kitanzania kulinda haki za wanawake na watoto  walio na  maambukizi ya maradhi ya Ukimwi kuhakikisha wanaishi kwa amani na utulivu katika familia zao.

Mpanju ametoa kauli hiyo hii leo wakati akihutubia wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwenye maadhimisho ya Siku ya UKIMWI yaliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya posta ya zamani mjini Ngara
PICHANI JUU NI KIKUNDI CHA NGOMA YA ASILI KUTOKA KUMNAZI WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA. 


"Baadhi ya watu wameingiliwa na mapepo kama ni mgeni au ndugu ukamkaribisha katika chumba cha watoto anaweza kuwafanyia vitendo vya kikatili na kuwaharibu maumbile  na kuwathiri kisaikolojia" Amesema Mpanju.
PICHANI JUU NI KIKUNDI CHA NGOMA CHA AKINA MAMA WA NYAMIAGA WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA.

Maadhimisho ya Ukimwi katika mkoa wa Kagera yamefanyika katika viwanja vya posta ya zamani vikitawaliwa na burudani za aina mbalimbali hasa vikundi vya ngoma na nyimbo chini ya  wakuu wa idara za serikali  na mashirika ya kutetea haki za binadamu kisheria.

Post a Comment

0 Comments