habari Mpya


Eneo la Lusahunga hadi Nyabugombe wilayani Biharamulo mkoani Kagera linavyotesa Magari na Abiria.

Eneo la barabara kuu kutoka Lusahunga mpaka Nyabugombe wilayani Biharamulo mkoani Kagera kwa muda mrefu limekuwa korofi kutokana na kukosekana kwa matengenezo ya uhakika katika barabara hiyo muhimu kibiashara kati ya nchi za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi.

 Magari mara kwa mara utayakuta yakiwa yamekwama kwa sababu ya ubovu hiyo na baadhi ya magari makubwa ya mizigo yanayopita  yakipata ajali kwa kushindwa kupanda  mlima vyema hali inayosababisha wakati mwingine foleni.
Hapa Kutaga kwa sana ,Magari hayo yamekwama kwa kuharibika au kushindwa kupita baada ya barabara kuzibwa na magari yaliyokwama.

Post a Comment

0 Comments