habari Mpya


Dkt Bashiru Ally -Aagiza Wizara ya Kilimo na Ushirika Kulipa Wakulima wa Kahawa Kagera.

Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally.

 Na Shaaban Ndyamukama RK.

 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally ameagiza Wizara ya Kilimo na Ushirika kupitia Naibu Waziri wa Wizara hiyo Visent Bashungwa kutafuta fedha  za kuwalipa wakulima wa zao la kahawa mkoani Kagera kwa bei inayoridhisha kulingana na gharama watumiazo katika uzalishaji.

Dkt Bashiru Ally aetoa agizo hilo mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa huo  wanaotoka wilaya ya Ngara Kyerwa na Karagwe katika kikao cha kazi juzi na kwamba haiwezekani wakulima waendelee kutaabika kukosa fedha wakati kahawa yao inashikiliwa na vyama vya ushirika

Amesema pia licha ya serikali kuzuia magendo ya kahawa kutoka kagera kuingia nchini Uganda lakini kahawa inanunuliwa kiuficho kisha inasafirishwa ikifungwa ndani ya kasha au kopo la robo kilo   hadi nje ya nchi hiyo inakuwa na thamani kubwa katika soko la kibiashara nchini China.

"Waganda wananunua kahawa kwa magendo wanaikaanga na kuifunga kwa kuweka picha ya mwanamke mrembo wa kiganda, wanaisafirisha hadi China kupitia bandari yetu inauzwa kakopo sh40,000 iweje mkulima apatiwe Sh1,000"? Alihoji Dkt Bashiru

Pia ameagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ngara Aidan Bahama kusitisha zoezi la kupora ardhi kuwanyanganya wananchi wa wilaya hiyo kwa madai ya kuwagawia wawekezaji kutoka Korea kusini.

" Nilikupigia simu kukuzuia sasa nakupa live sitaki kusikia wawekezaji wa nje wanaopewa ardhi bila kufuata utaratibu wa kuridhiwa kwanza na mikutano mikuu ya vijiji" Alisema Dkt Bashiru

Halmashauri ya wilaya ya Ngara imetoa ardhi zaidi ya ekari 10,000 kwa wawekezaji wa Korea kusini, wanaotaka  kuendesha kilimo cha zao la buni wakiahidi  kujenga kiwanda cha kahawa na mbolea huku wakilima mazao ya matunda zikiwemo aina za mbogamboga wilayani humo.

Wawekezaji wengine kutoka  Kuwait wamefika kukagua mabonde ya kilimo cha mpunga ambapo hawajaanza shughuli zao hadi serikali ikamilishe upembuzi yakinifu wa kupata maeneo hitajika na kuwashirikisha wananchi.

Vile vile aliwataka viongozi  wa chama na serikali kuhamasisha wananchi kufanya kazi lakini wakitumia vyakula vyenye kuzuia utapia mlo kwa watoto kiandaa wataalamu watakaoridhi nafasi zao na kwamba mkoa wa kagera unao watoto wenye utapiamlo asilimia 40.

Awali Mbunge wa Jimbo la Ngara Alex Gashaza alisema utaratibu wa kutoa maeneo ya ardhi ya kijiji cha kazingati ni ekari 8,000 na wataalamu walibainisha kuwepo ekari 4,000 lakini kijiji kitabaki bila maeneo ya kilimo na mifugo

Alisema kiutaratibu uwekezaji kulitakiwa kuitisha mikutano ya vijiji, kwa mujibu wa sheria namba tano ya ardhi ya mwaka 1999 na kwamba katika kutafuta eneo la havikufanyika vikao vya serikali ya kijiji na mkutano mkuu kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano (MOU)

"Pamoja na hayo havikufanyika vikao vya halmashauri kupitia baraza la madiwani Mimi nikiwa mjumbe sikupata taarifa wala kushirikishwa popote" Alisema Gashaza

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema wananchi wanahamasishwa kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya afya ambapo katika wilaya ya Kyerwa itajengwa Hospitality ya wilaya kwa fedha zinazotoka serikalini huku vikiboreshwa vituo vya afya na zahanati

Brigedia Jenerali Gaguti amesema katika kupambana na biashara ya magendo ya zao la kahawa wilaya ya misenyi imekamata magari 12 yenye tani zaidi ya 60 na pikipiki zilizosafirisha kahawa kwenda nchini Uganda na wamiliki wa vyimbo hivyo wametozwa faini Sh68 milioni na kahawa kutaifishwa.

"Fedha hiyo ilitumika kuimarisha ulinzi na usalama lakini pia kiasi kingine kiligawiwa halmadhauri ya wilaya ya Misenyi kuboresha miundombinu katika huduma za kijamii" Alisema Gaguti

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi waliohudhuria  kikao cha Katibu mkuu, walikuwa na maoni tofauti baadhi wakipongeza kauli yake ya kuzuia wawekezaji, wengine wakilalamika kwamba mkoa utakosa fursa za ajira kupitia miradi ya  wawekezaji wanaokuja.

Post a Comment

0 Comments