habari Mpya


Diwani na Wananchi Murukulazo Itazameni kwa Jicho la Huruma Shule ya Msingi Rusumo,Ngara.

Na Shaaban Ndyamukama - RK Ngara 97.9

Wazazi na wananchi wa kijiji cha Kyenda,  kata ya Mulukulazo wilayani Ngara mkoa wa Kagera wametakiwa kujitolea shilingi 2,000 kila kaya   kuchangia ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa ya  shule ya msingi Rusumo  vilivyoezuliwa na upepo tangu mwezi Agosti mwaka huu,2018.

Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho  Moses Gwihangwe amesema zaidi ya shilingi laki saba (Tsh700,000) zinahitajika  ili  kununua mabati 29 na mbao pamoja na misumari ikiwemo fedha ya kuwalipa mafundi watakaokarabati madarasa hayo.
Aidha Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo  William Ndabalokotse amesema  licha ya  madarasa hayo kuezuliwa  hakuna uongozi wa wilaya uliofika shuleni hapo   huku kukiwa na tetezi  kwamba  shule hiyo itahamishwa kupisha ili ujenzi wa miradi ya maendeleo ya  maporomoko  ya    Rusumo.

Tumewaita wazazi na walezi kujadili jinsi ya kupata fedha za kuchangia ukarabati wa vyumba vya madarasa changamoto inayojitokeza ni kutokuwa na maneno ya kwamba shule hiyo itahamishwa kwenye eneo la shule hii ilipo kwa sasa” Alisema Ndabalokotse.
Naye  Mwalimu Mkuu Wa Shule ya Msingi Rusumo   Iman Braiton Gashaza amesema madarasa yaliyoezuliwa  yalitumika kwa darasa la tatu hadi la sita  na kwamba hivi sasa Wanafunzi wanasomea nje licha ya kuwepo  majira ya mvua na jua.

Aidha Wanafunzi wanasomea kwenye  madarasa yaliyo wazi kwenye paa  na    wanaoteseka ni 450  na kwamba shule hiyo inahitaji vyumba vinanane vya madarasa baada ya vilivyopo saba kuonesha nyufa baada kuezuliwa kipindi cha mwanzo na kufanyiwa ukarabati lakini haviko imara

Shule hii inao  wanafunzi  719   na walimu 12 lakini zinahitajika nyumba 10 za walimu kwa kuwa  wanaofundisha hapa  wanaishi umbali wa kilomita  nne huko  Rusumo  wakipanga mitaani na wanalazimika kusafiri kwa mitumbwi  kuvuka mto Ruvubu” Alisema Imani Gashaza.
Vile vile amesema wanafunzi wanahitaji kutumia 20 lakini yaliyopo ni 10 pekee ambayo siyo imara huku akihimiza wananchi wa kijiji cha Kyenda kujitolea wakijua wanapaswa kukarabati miundombinu ya shule kwa ajili ya watoto wao na shule hiyo ni mali ya jamii ikipata nguvu kutoka serikalini.

Pia amekiri kuwepo tetesi za shule hiyo kuhamishwa kupisha miradi ya maendeleo  inayoendeshwa katika maporomoko ya mto Rusumo  lakini amedai hakuna maandishi yanayoweza kuthibitisha kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngara inayofahamu kuwepo miradi huko Rusumo.

Post a Comment

0 Comments