habari Mpya


DC Kahama Ataka Polisi Kufanyia Kazi haraka Taarifa za Ukatili wa Kijinsia.

Na Simon Dioniz –RK Kahama 97.3

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga amelitaka Jeshi la Polisi wilayani humo kuhakikisha wanazifanyia kazi taarifa zote zilizowasilishwa kuhusu ukatili wa kijinsia.

Akizungumza wakati wa kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wilayani Kahama December 10,2018 , Bw Anamringi Macha amesema tatizo la vitendo vya ukatili vimeshamiri kwa kiasi kikubwa.
Awali akitoa taarifa ya hali ya Ukatili tangu Januari mpaka Novemba mwaka huu Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya mji huo Bw Robart Kwela amesema hadi sasa watu zaidi ya 1,300 wamefanyiwa ukatili.

SIKILIZA TAARIFA YA SIMON DIONIZ KUTOKA KAHAMA.

Post a Comment

0 Comments