habari Mpya


Billion 1.58 zahitajika Kujenga Vyumba 79 vya Madarasa ya Sekondari Muleba.

Picha kabla na baada ya Ujenzi wa Darasa jipya katika Shule ya Msingi Kabalenzi iliyopo Bukoba Vijijini mkoani Kagera ikiwa ni zawadi ya kuboreshewa miundombinu iliyotolewa na Shirika la Jambo Bukoba la mkoani Kagera baada ya kushiriki katika mashindano ya Michezo ya Jambo Bukoba inayohusu stadi za maisha,katika Bonanza la mkoa 2018.

Shirika la Jambo Bukoba ambalo si la kiserikali limekua likisaida Juhudi za Mkoa wa Kagera kuboresha miundombinu mbalimbali ya Shule hasa za Msingi.

Ujenzi wa Madarasa ukiendelea,Muleba,Kagera.

Na Shafiru Yusuf –RK Muleba.

Zaidi ya shilingi billion 1.58 zinahitajika kwa ajili ya kujenga vyumba 79 vya madarasa vya shule za Sekondari zilizpo wilayani Muleba mkoani Kagera. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya wilaya ya Muleba Bw Emmanuel Sherembi katika taarifa yake kwenye harambe ya uchangiaji wa vyumba vya madarasa iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa halimashauri hiyo, amesema kuwa jumla ya Wanafunzi 9636 wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza 2019 huku wanafunzi 3966 wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa, hivyo amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha wananusuru wanafunzi hao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango amesema Jumla ya shilingi milioni 42,946,000 zimepatikana kwenye uzinduzi wa harambee, kati ya fedha hiyo pesa tasilimu iliyokusanya ni shilingi milioni 16,756,000  ,ahadi ni shilingi milioni 22,740,000  pamoja na vifaa vyenye thamani ya shilingi million 3,280,000.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Muleba Bw Krizanti Kamugisha amewaagiza watendaji wa vijiji na kata kuwasomea mapato na matumizi wananchi pale wanapokuwa wamekusanya fedha mbalimbali za wananchi.

Post a Comment

0 Comments