habari Mpya


Akutwa Amefariki huku Gari lake Likiwa Limepinduka -Bukoba.

Gari eneo la ajali.
Na Anord Kailembo – RK Bukoba 97.7

Mwanaume Lameck Anord aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Carina, amekutwa amefariki kwenye mteremko wa barabara ya Kashura Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera huku gari lake likiwa limepinduka.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera Revocatus Kasanga ameiambia redio Kwizera kuwa, tukio hilo limetokea asubuhi ya December 12, 2018, na uchunguzi wa awali umebaini dereva huyo aliacha njia wakati akikata kona ya kutokea Kashura na kutelemka mjini kutokana na mwendokasi.

Amesema kuwa wamepokea taarifa za kwamba dereva huyo alikuwa amebeba wanawake 2 wakisafirisha Samaki lakini watu hao sambamba na samaki hawakukutwa kwenye gari hilo na hatua za kuwabaini ili wasaidie katika uchunguzi zinaendelea.

Post a Comment

0 Comments