habari Mpya


Zingatieni Matumizi Sahihi ya Ruzuku Kadili ya Malengo ya TASAF III.

Walengwa wa malipo ya dirisha la kipindi cha Septemba – Oktoba 2018 wa TASAF III katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya ruzuku walizopokea, ili watimize lengo la mpango wa TASAF III, ambalo ni kuwawezesha kujiongezea kipato.

Afisa Ufuatiliaji Mradi wa TASAF III Ndugu Frank L. Anthony, amesema Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imekamilisha malipo ya ruzuku dirisha la septemba – Oktoba 2018, lililofunguliwa Oktoba 07, 2018 na kukamilika Oktoba 12, 2018.

Niwaombe walengwa wote kufanya matumizi sahihi ya ruzuku, waliopokea kama lilivyo lengo la mpango huo, amablo ni kuwapa uwezo walengwa waweze kujikwamua katika lindi la umasikini, na kujiongezea kipata kwa kujishughulisha kiuchumi.” Alisema Ndugu Anthony.

hata imthibitika kwamba watu wapatao 10 hawakujitokeza kwenye dirisha lililokamilika, kwa sababu mbalimbali ikiwemo kusafiri, ugonjwa, kuhama na hata wengine kuaga dunia, lakini taarifa zao zimehifadhiwa.

WaLengwa 10 ambao hawakupata malipo dirisha hili, watapata haki yao katika dirisha linalokwenda kuanza mwishoni mwa Novemba 2018, na kukamilika mwanzoni mwa Desemba 2018, na kwamba waliojitokeza katika malipo hayo walikuwa 7738 kati ya 7748.

Amesema kwamba kiasi cha shilingi 220,000/= zimerejeshwa makao makuu ya TASAF baada ya walengwa hao kutojitokeza; na kuongeza kuwa walengwa hao wajitokeza siku ya malipo, ili kupata maelekezo na mafunzo stahiki juu ya matumizi ya fedha.

Katika Dirisha la Sepemba – Oktoba 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imepokea jumla ya shilingi 279,660,500.00, kwa ajili ya malipo ya ruzuku kwa kaya masikini na uwezeshaji wa zoezi hilo.

Tumepokea shilingi 259,700,000.00, kwa ajili ya ruzuku kwa kaya maskini zipatazo 7748 kutoka katika vijiji 52 vilivyo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini - TASAF III, zoezi hili litaaanza mara tu taratibu za kifedha zitakapokamilika.” Alisema Ndugu Anthony.

Aidha, katika kiasi kilichopokelewa, shilingi 5,200,000.00; zitatumika kwa ajili ya uwezeshaji wa malipo ngazi ya kijiji, ambapo kila kijiji kitapokea shilingi 100,000.00 kama malipo kwa wenyeviti, watendaji, wajumbe watatu ngazi ya kijiji pamoja na mjumbe wa kamati ya usimamizi wa mradi ngazi ya jamii (CMC).

Ndugu Anthony amesema kiasi cha shilingi 13,980,500.00, kitatumika kwa ajili ya kuwezesha zoezi la kuhawilisha fedha kutoka Halmashauri kwenda katika kila kijiji kulichomo katika  mpango.

Alifafanua kwamba kiasi cha shilingi 780.000.00, kitatumika kuwezesha shughuli za mpango na zoezi la malipo ngazi ya kata, ambalo linawahusisha waratibu elimu kata, maafisa ugani na wauguzi wanaohusika kujaza fomu za masharti ya afya kwa walengwa.

Post a Comment

0 Comments