habari Mpya


Ngara-Murusagamba na Nterungwe Vinara wa Lishe Duni kwa Watoto.

Tatizo hili  linarudisha nyuma maendeleo ya wilaya Ngara,mkoa wa Kagera  na  taifa   kwa kiasi kikubwa, hali hii inapelekea kutokufikia kwa malengo ya dira ya maendeleo ya taifa  kwani athari  zinazotokana na tatizo la Utapiamlo ni  watoto kupugua uzito mara kwa mara, vifo  na ukuaji duni kimwili na kiakili.(Picha na Maktaba yetu)


Moja  ya sababu kubwa inayochangia  tatizo la utapiamlo katika wilaya ya Ngara ni kukosekana  kwa elimu sahihi kuhusu umuhimu wa lishe ya watoto wachanga na wadogo pia kuto kutambua umuhimu wa lishe kwa wanawake  wajauzito na baada ya kujifungua na kuwalisha watoto vyakula kabla kufikia umri wa miezi sita.
Watoto walio chini ya umri wa miaka miwili wanakabiliwa na utapiamlo kwa wastani wa asilimia 45 katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera kutokana na wazazi au walezi kutowapatia vyakula vyenye vitamini pamoja na protini.Afisa lishe wilayani Ngara Bw John Sostenes amesema ili kukabiliana na hali hiyo wazazi na walezi watumie vyakula vya asili vinavyopatikana kwenye mazingira yanayowazunguka kuwakinga watoto wao kupata udumavu wa mwili na akili.Pia amesema baadhi ya vijiji katika halmashauri ya wilaya ya Ngara vimekuwa na utapiamlo wa asilimia 10 hadi 50 hali ambayo ni mbaya licha ya kuwa na vyakula vinavyotumika kuongeza vitamini na protini.Naye Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara ambaye pia ni Afisa elimu idara ya msingi wilayani humo  Bw. Gidion Mwesiga  amewahimiza walimu kuhamasisha wazazi  na walezi kuchangia nafaka za aina mbalimbali kuwezesha upatikanaji wa uji shuleni ili kuwakinga wanafunzi na njaa kwa siku  nzima.

Post a Comment

0 Comments