habari Mpya


Waziri Mhagama Aonya Kutotumia Kituo Cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama Kutaka Faida.

Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye Ulemavu ,Bi. Jenista Mhagama akimkabidhi Meneja wa NSSF Kahama Bw. Winston Mundigile Ufunguo wa Ofisi Ndogo alipofungua rasmi kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
 Taasisi mbalimbali zimepewa ofisi ndogo ili kutoa elimu na rasilimali nyingine ili kuwakwamua wananchi wa Wilaya ya Kahama Kiuchumi.

Na Simon Dioniz -RK Kahama 97.3
Serikali imedhamilia kuondoa vikwazo ambavyo vimekuwa vikichangia wananchi kutoendelea kiuchumi hasa katika bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali kwa kukosa mitaji, ujuzi na ubunifu katika uendeshaji wa shughuli zao.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi, Mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Festus Limbu amesema kuwa vikwazo vinavyowakwamisha wananchi kutofanikiwa ni kuhakikisha vinaondolewa kwa kuwajengea uwezo wananchi na kuwapa mbinu ili waweze kufanikiwa. 

BOFYA KUSIKILIZA HAPA

Akizungumza baada ya kuzindua kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi wilayani Kahama, Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye Ulemavu ,Bi. Jenista Mhagama amezionya taasisi za kifedha kutotumia kituo hicho kutaka faida kupitia kwa wananchi ambao watakuwa wanafika kwa ajili ya kuhitaji mikopo. 

BOFYA KUSIKILIZA HAPA


Aidha ,Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa serikali haiwezi kuvumilia kuona watu wanashindwa kupata mikopo kutokana na kupandishwa kwa liba na kuahidi kuwa sula hilo atalisimamia mwenyewe ili kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments