habari Mpya


Watatu Wahukumiwa Kunyongwa Kesi ya Bigira Thadeo –Kagera.

Jengo la mahakama kuu Bukoba ambalo lilizinduliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati huo Jakaya Kikwete tarehe 25/07/2013. -Picha na Maktaba Yetu.

Na William Mpanju- Biharamulo.

Mahakama kuu kanda ya  Bukoba Mkoani  Kagera  imewahukumu  watu 3  wakazi kijiji cha  Kashinga  Wilayani Ngara  kunyongwa  hadi kufa baada ya kupatikana  na hatia ya kuuwa kwa kukusudia.

Jaji wa mahakama kuu  ya Tanzania  kanda ya Bukoba  Rusia  Kairo   kabla  ya kutoa hukumu hiyo  amewataja washitakiwa  hao  kuwa   ni Minani  John  mwenye umri wa miaka 25,  Dionizi  Gervas  mwenye umri wa miaka 29, William Julias  Mwenye umri wa miaka 28 wote wakazi wa kijiji cha Kashinga wilayani Ngara.

Akisoma hukumu hiyo mbele ya wakili  wa serikali  Haruna  Shomari  na Mawakili  Wawili, upande wa utetezi   Chiristiani Vyamungu na Aneth Rwiza,  Jaji Kairo ameiambia Mahakama kuwa washitakiwa  kwa pamoja  mnamo  August 1 mwaka 2014  katika kitongoji cha Mubitasha kijiji cha Kashinga    walimuuwa kwa makusudi Bigira Thadeo.  

Jaji  Kairo  amesema  mahakama  imeridhika  na ushahidi upande  wa Jamuhuri kuwa washitakiwa  3 kati ya 4  ndio wamehusika  na kifo cha marehemu Bigira Thadeo ,hivyo  mahakama  imewahukumu   kunyongwa hadi kufa  huku  ikimwachia huru mtuhumiwa  Jacob Sigiri baada ya kubainika kuwa hakuwepo siku ya tukio.

Post a Comment

0 Comments