habari Mpya


Wananchi Kasulu - Madiwani wanaojiuzulu Hawana Mchango wa Maendeleo Katani.

 Na Philmon Golkanus –RK Kasulu 94.2

Baadhi ya Wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamesema hali ya kujiuzulu kwa baadhi ya madiwani wilayani humo ni sahihi kutokana na kutoonesha mchango wa maendeleo katika kata zao toka waingie madarakani.

Wakizungumza na Radio Kwizera, wamesema pamoja na viongozi hao kuwepo madarakani kwa miaka mitatu sasa, hakuna juhudi za maendeleo zinazoonekana katika maeneo yao na hivyo wananchi wanaunga mkono hatua za kujiudhuru kwao.


BOFYA KUSIKILIZA HAPA
Hivi karibuni madiwani wa kata tatu za halmashauri ya mji na wilaya ya kasulu wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na chama cha mapinduzi na kata zao kubaki wazi bila uwakilishi katika mabaraza ya halmashauri.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kasulu Bw. Abdallah Mbelwa amethibitisha kuwapokea Bw. Evance Buchonko wa Kata ya Msambara kupitia ACT Wazalendo, Bw. Ayubu Ngaraba Kata ya Kigondo na Bw. Eliya Kagoma Kata ya Kitanga wote Kupitia NCCR-MAGEUZI.

Post a Comment

0 Comments