habari Mpya


Wananchi Biharamulo wamvaa Mbunge wao Kwa Kushindwa Kuwatembelea.

Stendi Kuu ya Mabasi Biharamulo Mjini.

Na Wiliam Mpanju –RK Biharamulo 97.9


Baadhi ya wakaazi wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamemlalamikia mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi Bw.  Oscar  Mkasa kwa kushindwa  kuwatembelea  tangu  wamchague mwaka 2015  ili waweze kumueleza  kero zinazowakabili na kuzifikisha  panapohusika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti na RADIO KWIZERA, wananchi wa vijiji vya Rugondo, Nyambale na Biharamulo mjini wamesema wanaowatembelea wananchi ni madiwani lakini mbunge hawajawahi kumuona tangu wamchague.

Wamesema  walitumia  haki yao ya msingi ya kumpigia kura wakiamini kabla ya kwenda kuwawakilisha bungeni atawatembelea ili kubaini  kero zao hasa za ukosefu wa maji safi na salama, barabara kwa baadhi ya vijiji na pembejeo za kilimo  ili kuzitafutia ufumbuzi.


BOFYA KUSIKILIZA WANANCHI 
Akijibu malalamiko ya wananchi hao, mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi Bw. Oscar Mkasa amesema amekuwa akitembelea baadhi ya kata za wilaya ya Biharamulo anapokuwa jimboni na kwamba kwa sasa yupo Dar es salam Kikazi hivyo ziara ya kutembelea kata itaanza mwezi Disemba mwaka huu baada ya vikao vya Bunge Mjini Dodoma kumalizika.

BOFYA KUSIKILIZA MAJIBU YA BW. MKASA

Post a Comment

0 Comments