habari Mpya


Wafanyabiashara wanaochakachua Bidhaa wakalia Kuti Kavu Kahama.

Hivi karibuni,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi.Zainab Telack aliwaonya maofisa wa TRA kuacha mara moja tabia ya kuwalinda wafanyabiashara wanaotakatisha na kuchakachua bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ikiwemo sukari,unga na mafuta ya kupikia.

Na Simon Dioniz RK Kahama 97.3

Kufuatia zoezi la Kukagua uchakachuaji wa bidhaa za Biashara kwenye maduka mkoani Shinyanga, Mamlaka ya vipimo Tanzania tawi la Kahama limeanza zoezi la kukagua bidhaa ambazo zinauzwa bila kufikia kiwango halisi cha kipimo na wale ambao watabainika watachukuliwa hatua


Meneja wa vipimo mkoani Shinyanga  Bw. MANENO POPATI amesema kuwa zoezi hilo linafanywa nchi nzima na kwa mkoa wa Shinyanga linafanyika katika  halmashauri zote za mkoa ambapo watakagua kila duka na kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa maduka ya jumla


Amesema kuwa kuna tabia ya watu kununua bila kupimiwa hali ambayo imekuwa ikichangia wafanyabiashara wadogo kupata hasara kubwa pamoja na wakulima na wavuvi kwani vipimo wanavyotumia ni batili Kutokana na hali hiyo Meneja wa vipimo mkoani Shinyanga Bw. Maneno Popati amewataka wafanya biashara kutumia vipimo halisi ambavyo ni Mzani

Post a Comment

0 Comments