habari Mpya


Utoaji wa Elimu ya Usalama Barabarani kwa Madereva wapunguza Tatizo la Ajali Kigoma.

Na Adrian Eustaus RK Kigoma 94.2

Utoaji wa elimu ya usalama barabarani kwa Madereva Mkoani Kigoma imetajwa kuwa moja ya njia zinazosaidia  kuwepo kwa matumizi bora ya barabara  na kupunguza ukubwa wa tatizo la ajali za barabarani mkoani humo. 

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani  mkoani Kigoma BW. MALEGE KILAKALA amesema hayo katika mahojiano na Radio Kwizera na kufafanua madereva na watumiaji wengine wa barabara wamefundishwa dhana ya matumizi bora ya barabara na sheria zake.

Amesema mkakati huo umesaidia kupunguza ajali ambapo ajali 30 zimetokea kuanzia Januari hadi Septemba 2018 na kusababisha vifo vya watu 33 ikilinganishwa  na mwezi January hadi September  2017 ambapo watu 59 walifariki. 


 Kwa upande wao baadhi ya madereva wa vyombo vya moto mkoani Kigoma kupitia umoja  wa chama chao  watashirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usama barabarani  kuripoti,kutoa taarifa na elimu ili kupunguza ajali.

Post a Comment

0 Comments