habari Mpya


TMA Kagera yataka Kupuuzwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii Kunyesha Mvua Zinazoweza Kusababisha Mafuriko.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba 97.7

Mamlaka ya hali ya Hewa nchini TMA mkoani Kagera imewataka wakazi wa mkoa huo kupuuza taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kunyesha kwa mvua kubwa zinazoweza kusababisha mafuriko.

Akizungumza na radio kwizera Meneja wa mamlaka hiyo mkoani Kagera Bw STIVIN MARUNDO amesema kuwa  hakuna utabiri unaoonesha mkoa wa Kagera kutarajia kupata mvua kubwa ,isipokuwa utabiri unaonesha mvua za msimu wa vuli kuwa chini ya kiwango kilichozoeleka.

Amesema kuwa taarifa za mamlaka ya hali ya hewa zinatoa tahadhali kwa jamii hutolewa kupitia vyombo vya habari  na kwenye vyanzo rasmi  vya mawasiliano  vya mamlaka hiyo  na kwamba ikitokea imetuma taarifa kupitia mitandao ya kijamii taarifa hiyo huwa na nembo ya mamlaka ya hali ya hewa nchini.
Picha na Maktaba yetu.Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamesema kuwa ipo haja ya mamlaka ya hali ya hewa  kubainisha vyanzo vya taarifa zake  kwa wananchi ili iwe rahisi kwao kuvitumia.

Post a Comment

0 Comments