habari Mpya


Samaki Tani 1.2 wa Milioni 10, Wakamatwa na Idara ya Vuvuvi Kagera.

Idara ya uvuvi mkoani Kagera imekamata samaki aina ya sangara  tani 1.2 wenye thamani ya Shilingi  milioni 10 na elfu 39 ambao wamepatikana kwa njia ya  uvuvi usiofata utaratibu.
Ofisa Mfawidhi ulinzi wa rasilimali za Uvuvi mkoani Kagera Bw.WEST MBEMBATI katika taarifa yake kwa waandishi wa habari, amesema samaki hao walikuwa wakitoroshwa kwenda nchini Uganda.

Bw.MBEMBATI amesema  kati ya samaki hao wapo ambao walivuliwa wakiwa chini ya sentimita 50 na wengine zaidi ya sentimita 85 wanaoruhusiwa kwa mujibu wa sheria .

Naye Ofisa Mfawidhi ulinzi wa rasilimali za Uvuvi kanda ya Ziwa victoria DIDAS MTAMBALIKE amesema  Samaki hao wamegawiwa kwa taasisi mbalimbali zikiwemo baadhi ya shule za msingi na sekondari manispaa ya Bukoba.

Post a Comment

0 Comments