habari Mpya


Rais Magufuli –Sasa Korosho Itanunuliwa na Serikali kwa sh 3,300.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli  amegoma Makampuni Kununua Korosho ya Wakulima katika mikoa ya kusini ,kwa madai ni wababaishaji na wanataka kuwaibia wananchi.
 
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo November 12,2018 wakati wa zoezi la kuwaapisha Mawaziri wapya walioteuliwa na kusema kwamba Serikali itanunua korosho  yote kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo.

Awali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba kuna makampuni 13 yamejitokeza kutaka kununua korosho kwa bei elekezi ya tsh. 3000

Aliyataja makampuni hayo kuwa  ni Mega movers  ambayo inataka tani laki 2, kampuni ya Kitanzania Mkeme Agri inataka tani elfu 5, na makampuni matatu yatachukua tani elfu 5, makampuni manne, tani elfu moja moja.

Ombi hilo limekataliwa na Rais Magufuli kwa madai kwamba  wafanyabiashara hao  ni wababaishaji, hivyo korosho yote itanunuliwa na serikali kwa sh 3,300 kwa kilo isiyobanguliwa.

Post a Comment

0 Comments