habari Mpya


Mfanyakazi TTCL Shinyanga Afariki kwa Kupigwa Jiwe na Mumewe.

Na Simon Dioniz –RK Kahama 97.3

Mfanyakazi wa Kampuni ya simu TTCL mkoa wa Shinyanga Bi. BUPE JACOB miaka 48 amefariki dunia baada ya kupigwa jiwe kichwani na Mume wake SHYROCK KIMARO (48) mwendesha bodaboda mkazi wa Ibadakuli mjini Shinyanga.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga ACP ALCHELAUS MUTALEMWA,  tukio hilo limetokea Novemba 5, 2018 majira ya saa 12 jioni katika Mtaa wa Miti Mirefu, Kata ya Mjini, Manispaa Shinyang’a 

Amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina ya SHYROCK na mkewe BUPE ambao walitengana hivi karibuni.
Kamanda MUTALEMWA amesema kuwa Siku ya Tukio Marehemu BUPE alimpigia simu Mume wake akiomba matumizi ya mtoto Lakini walipokutana alimsukuma na kuanguka , ndipo alipompiga jiwe kichwani na kufariki papo hapo.

Polisi inamshikilia Mtuhumiwa na atafikishwa Mahakamani.

Post a Comment

0 Comments