habari Mpya


Mamlaka ya Maji Ngara Yashauriwa Kuomba Kibali cha Kutumia Mil 24 Kuboresha Huduma.

Na Shaban Ndyamukama- RK Ngara.

Mamlaka ya maji kwenye Halmashauri ya wilayani ya Ngara mkoani Kagera imeshauriwa kuandika barua ya kuomba upya kibali kwa wizara ya maji kutumia shilingi milioni 24 zilizotolewa na Serikali wilayani Ngara ili kuboresha miundombinu katika mji wa Ngara kupunguza changamoto ya maji kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Maji mijini kutoka Wizara ya Maji, Mhandisi William Christian ametoa ushauri huo wakati akipokea taarifa ya changamoto ya huduma ya maji katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ngara akiwa ziarani kufuatilia upatikanaji wa huduma hiyo.
 
Bw Christian ameitaka halmashauri hiyo iandike barua ya kuomba fedha za kujenga visima vipya vya maji kiasi cha shilingi milioni 200 hadi 300 kwa ajili ya kuongeza huduma ya maji wilayani Ngara na maeneo jirani.

Hata hivyo kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Gidioni Mwesiga ameomba Wizara kuingilia kati madeni ya taasisi zinazodaiwa na mamlaka hiyo zaidi ya shilingi milioni 18 kwani zikipatikana zinaweza kusaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazojitokeza.

Post a Comment

0 Comments