habari Mpya


Mama Mzazi Aua na Kujeruhi Wanae kwa Dawa ya Kienyeji Buhigwe.

Na Philmon Golkanus –RK Buhigwe,Kigoma 94.2.

Mtoto mmoja amefariki na wengine wanne wamelaza hospitalini  baada ya kunywa dawa ya kienyeji waliyopatiwa na Mama yao Mzazi katika kitongoji cha Munyika kijiji na kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.


Mtoto mmoja kati ya watoto hao waliolazwa katika Hospitali ya Mlimani wilayani Kasulu mkoani Kigoma Melkizedek Hamenya, amesema mama yao aliwakorogea dawa hiyo kwenye kikombe na kuwalazimisha kunywa huku akiwatishia kwamba endapo wasipokunywa atawafukuza.

 BOFYA PLAY KUSIKILIZA HAPA CHINI

Mganga Mfawidhi wa Kituo Cha Afya Muyama Joachim Kulwa amethibitisha kuwapokewa watoto wanne ambao baada ya kuwafanyia uchunguzi waligundulika wametumia dawa za kienyeji zilizopelekea wao kuvimba tumbo na miguu na kuamua kuwapa rufaa kwenda Hospitali ya Mliman.

Imeelezwa kuwa mama huyo Bi.Varelia Timba aliwapa dawa watoto wake kwa lengo la kuwafanya wamsahau Baba yao mzazi.

Akiwauguza hospitalini hapo, shangazi wa watoto hao Bi. Pelesi Yusuph, mama huyo alitengana na mume wake miaka mitano sasa kwa madai kuwa ni mgonjwa na inasadikika kuwa kwa sasa ana mahusiano na shemeji yake ambaye hakutaka kumuoa akiwa na familia.

BOFYA PLAY KUSIKILIZA HAPA CHINI
Diwani wa kata ya Kajana Bw. Robson Ngeze amesema mama huyo anayedaiwa kuwapa dawa watoto hao, ametoroka na kwamba kama Serikali wanaendelea kumtafuta ili wamchukulie hatua za kisheria.

Post a Comment

0 Comments