habari Mpya


Kigoma-‘’ Tatueni Migogoro ya Kijamii kwa Misingi ya Kisheria’’.

Washiriki wa Mafunzo.

Na Adrian Eustuce- RK Kigoma 94.2.

 Mafunzo rejea kwa Wasaidizi wa Kisheria mkoani Kigoma yanayofadhiliwa na Taasisi ya Legal Service Facility -LSF yamehitimishwa jana November 23,2018 na yalilenga kuwajengea uwezo Wasaidizi hao wa Kisheria katika Utatuzi Wa Migogoro mbalimbali ya Kijamii kwa kuzingatia misingi ya Sheria.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Afisa Tathimini na Ufuatiliaji kutoka Taasisi ya Bak Aids inayoratibu shughuli za Wasaidizi wa Kisheria mkoani Kigoma Bw. Hamis Karisha amewataka Wasaidizi wa Kisheria kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kutunza kumbukumbu za Wateja wanaopatiwa huduma katika ofisi zao. 
 
Wadau mbalimbali wa Masuala ya Kisheria nchini ikiwemo TLS, Shule ya Sheria Tanzania kupitia ofisi ya Msajiri wa huduma za Msaada wa Kisheria nchini wameahidi kuendelea kuzisaidia ofisi za msaada wa kisheria ili kuhakikisha jamii inahudumiwa kwa usawa na ubora unazingatia misingi ya Sheria za nchi.
 

Post a Comment

0 Comments