habari Mpya


Kanali NDAGALLA awataka Madiwani Kakonko Kujitathmini.

Na Faraja Marco- RK Kakonko.

Mkuu wa wilaya ya kakonko Mkoani Kigoma Kanali HOSEA NDAGALLA amewataka madiwani wa halimashauri hiyo kujitathmini ni nini ambacho wamekifanya kwa wananchi baada ya kuwachagua mwaka 2015.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali HOSEA NDAGALA akizungumza katika kikao Cha Baraza la Madiwani Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma November 7, 2018.

Akizungumza na madiwani kupitia kikao cha baraza la madiwani jana mjini Kakonko,Kanali NDAGALA amesema wapo baadhi ya madiwani ambao wameonyesha nia ya kuwatumikia wananchi  kwenye kata zao kwa vitendo  huku wengine  wakishindwa kutimiza wajibu wao kwa wananchi. 

Amesema hata vumilia wananchi wakiendele kupata kero mbalimbali  ikiwemo ukosefu wa madarasa,maji,na barabara  na lazima Madiwani waone umuhimu wao kuwa sehemu ya maendeleo  kwa ajili ya wananchi.
Baadhi ya Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kakonko.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri BW.MASUMBUKO STEFANO amesema watendaji wa idara mbalimbali sambamba  na madiwani kutimiza wajibu wao ili Kakonko kuwa na maendeleo endelevu.

Kwa upande wao Diwani Kata ya Mgunzu Bw.ENDREW MASHAMA na  wa kata ya Gwanumpu Bw.TOYI BUTONO  wameahidi kuwahamasisha  wananchi kushiriki kwa mshikamano  kufanya kazi kwa bidii

Post a Comment

0 Comments