habari Mpya


Kagera Tujenge na Kutumia Choo Bora.

Na Anord Kailembo na Wiliam Mpanju–RK Bukoba 97.7 

Wilayani Biharamulo mkoani Kagera, Zaidi ya Asilimia ya 39 ya wakaazi takriban elfu 22 wa wilaya hiyo hawana vyoo.

Kaimu Afisa Afya Na Usafi Wa Mazingira wilaya ya Biharamulo   Bw. Said Suleiman  amesema  miongoni mwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa ikiwemo kuwaagiza Watendaji wote wa Vijiji kwa kushirikiana na Maafisa  Afya na Wahudumu wa  Afya  ngazi za Vijiji kuhakikisha wanafanya ukaguzi kwa kila kaya  na watakaobainika kutokuwa na choo atozwe  shilingi elfu  50 kabla ya kumfikisha Mahakamani.

Nao baadhi ya Wakazi wa Biharamulo wamesema  hawana uwezo wa kujenga choo cha kisasa  kutokana na uwezo mdogo wa kifedha za kugharimia  vifaa vya ujenzi  wa choo bora  ikiwemo vifaa vya kiwandani

 Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Afya za November 19,2017, Tanzania ilikuwa na Kaya zenye vyoo bora asilimia  40 tu. Kaya zenye vifaa maalum (sabuni + maji) vya kunawa mikono ni 34% tu.

Kati ya shule za Msingi (16,088) zenye vyoo bora ni 28% tu.

Wilaya ya Njombe, zaidi ya asilimia 95% ya Kaya zina vyoo bora na sehemu maalum za kunawia mikono.
Tatizo la Kaya kutokuwa na Vyoo mkoani Kagera limetajwa kupungua kutoka Kaya elfu 7 hadi kaya elfu 3 kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu,2018.

Afisa Afya Mkoa Wa Kagera Bw. Nelson Lumbeli ameiambia Radio Kwizera kuwa kwa mkoa wa Kagera ni asilimia 54 ya kaya za zenye vyoo bora, 45 zina vyoo visivyo na sifa huku asilimia 1.3 hazina vyoo kabisa.

Amesema kuwa kupungua kwa kaya hizo kumetokana na uhamasishaji na ukaguzi wa mara kwa mara unazofanywa na maafisa pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali na kwamba kufikia Disemba mwaka huu serikali ya mkoa ina lengo la kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora

BOFYA KUSIKILIZA HAPA
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba wamekiri kuhamasishwa kujenga vyoo bora lakini changamoto kubwa inayokwamisha watu kujenga vyoo hivyo ni hali duni ya kipato wakidai kuwa choo bora kinahitaji gharama.

Post a Comment

0 Comments