habari Mpya


Halmashauri ya Ngara yadaiwa Milioni 40 na Mafundi Ujenzi Kituo cha Afya Murusagamba.

Jengo la Kituo cha Afya Murusagamba.

Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera, inadaiwa zaidi ya milioni 40 na Mafundi waliosaini mkataba wa kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Murusagamba.

Hilo limebainishwa na Mafundi saba walioshiriki katika ujenzi ambao wamefika katika ofisi za redio kwizera wakilalamika kutolipwa fedha zao.

SIKILIZA MALALAMIKO YAO HAPA.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara Dr. Revokatus Ndyekobora akizungumzia swala hilo amesema mafundi hao wamekwisha lipwa na wamebaki wanadai kiasi kidogo cha fedha ambapo mipango ya kuwalipa inaendele.

MAJIBU YA FEDHA ZA VIBARUA HAPA.
Kituo cha Afya Murusagamba kimefanyiwa upanuzi kwa kujengwa wodi na nyumba za watumishi na shilingi Milioni 400 zilitolewa na Serikali kufanya ukarabati huo.

Post a Comment

0 Comments