habari Mpya


Hakuna Changamoto yoyote Mtihani Kidato Cha Nne 2018 Ngara.

Jumla ya watahiniwa elfu 1 mia 8 na 92 wilayani Ngara mkoani Kagera wameungana na wenzao nchini kote kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya kidato cha nne .

Akizungumza na Radio Kwizera, Ofsini kwake Afisa Elimu Shule za Sekondari wilayani Ngara, Mwl Fikeni Senzige amesema mpaka sasa Watahiniwa wote wanafanya Mtihani na hakuna changamoto yoyote iliyo jitokeza katika vituo vyote vya kufanyia mtihani.
 
Mwl Senzige amewataka watahiniwa kujiamini wanapoendelea kufanya mitihani yao maana wameandaliwa vizuri ili kuhakikisha wanapata ufaulu mzuri.

Hata hivyo Mwl Senzige amewataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa watoto wao hasa katika kipindi hiki kwa kuwapatia mahitaji muhimu wanayohitaji wakiwa wanaendelea na mitihani yao.

Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), jumla ya watahiniwa 427,181 wamesajiliwa kufanya mtihani huo ambao utamalizika Novemba 23, 2018.
 
Watahiniwa wa Shule ni 368,227 na Watahiniwa wa Kujitegemea ni 58,954.

Kati ya Watahiniwa wa shule 368,227 Waliosajiliwa, Wanaume ni 180,908 sawa na asilimia 49.13 na Wanawake ni 187,319 sawa na asilimia 50.87.

Watahiniwa wenye Mahitaji maalum wapo 562 kati yao 372 ni wenye uoni hafifu, 44 wasioona, 109 wenye ulemavu wa kusikia na 37 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili.

Post a Comment

0 Comments