habari Mpya


Elimu Kikwazo cha Lishe Bora kwa Watoto Muleba.

Wataalamu wanasisitiza ulaji wa mlo kamili ili kuimarisha afya.

Na Shafiru Yusuf –RK Muleba.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kagasha Wilayani Muleba Mkoani Kagera wamelalamikia Serikali kwa kutowapa elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya lishe bora kwa watoto wao.

Wakizungumza na Redio Kwizera kwa nyakati tofauti wamesema hawana elimu yoyote ya matumizi sahihi ya lishe kwa watoto wao hali inayopelekea udumavu kwa watoto.
 
Wamesema endapo wakipewa elimu ya kutosha wataondokana na hali hiyo kwani kuna baadhi ya wazazi wanashindwa kuwahudumia watoto wao.
 

Kwa upande wake Afisa Lishe wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Bw Robison Tigelerwe amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara hasa kwenye vituo vya afya juu ya matumizi sahihi ya kulisha mtoto ingawa pamekuwa na mwitikio mdogo kwa wazazi pale wanapokuwa wanatoa elimu.
 

Hivi karibuni ripoti ya shirika la afya la kimataifa imebainisha kuwa mtu mmoja hufariki dunia katika watu watano kwa kukosa lishe bora huku Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umesema kuwa, kuna watoto milioni moja wana lishe duni barani Afrika.

Post a Comment

0 Comments