habari Mpya


DC Ruyango ampa Siku Saba Mkurugenzi na Afisa Uvuvi Muleba Kutoa Elimu na Kudhibiti Uvuvi Haramu.

Na Shafiru YusuF –RK Muleba.

Mkuu wa  ya wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Mhandisi RICHARD RUYANGO ametoa siku saba  kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bw EMANUEL SHELEMBI  pamoja na Afisa Uvuvi wa halimashauri Bw WILIFRED KIBENDELANA  kutoa taarifa ya udhibiti wa  vitendo vya uvuvi usiofata utaratibu  katika ziwa Burigi .

Mhandisi RICHARD RUYANGO  amesema  hayo katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika jana mjini muleba  na kwamba  Uvuvi usiofata sheria uendane na elimu kwa wavuvi  ili kunusuru mazalia ya samaki katika ziwa Burigi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Muleba Bw. EMMANUEL SHEREMBI amesema maagizo yaliyotolewa  atahakikisha yanatekelezwa huku akiwaagiza viongozi wa vijiji na kata kusimamia ipasavyo  maagizo yote ya kukomesha vitendo vya uvuvi usiofata utaratibu.

Post a Comment

0 Comments