habari Mpya


Damu Yahitajika Zaidi Ngara.

Na Shaaban Ndyamukama- RK Ngara.

Jamii imeombwa kujitolea kuchangia  damu kwenye vituo vya kutolea huduma za matibabu kwa kutanguliza moyo wa uzalendo  kuweza kunusuru maisha ya wenye mahitaji  hasa watoto wachanga  wakiwemo wajawazito  wanaokaribia  kujifungua

 Mratibu wa damu salama wilayani Ngara Bw Mugisha Joseph Lubagola amebainisha hayo  wakati akiongea na  Radio Kwizera akiwa katika zoezi la kuchangia damu Hospitali ya Murugwanza wilayani Ngara

Lubagola amesema  kwamba wilaya hiyo inahitaji chupa za damu zaidi ya 200 kila mwezi  kwa ajili ya hospitali tatu zinazohudumia wagonjwa wa aina mbalimbali ambazo ni Rulenge Murgwanza na Nyamiaga vikiwemo vituo vitatu vya afya.
Wagonjwa wanaohitaji damu ni watoto wachanga , wanawake wanaohitaji kujifungua na wanaopata ajali kutokana na matukio mbalimbali na msaada mkuba tunaupata kwa wanafunzi wa sekondari wanaojitolea” Amesema Lubagola.

Baadhi ya wagonjwa  katika hospitali ya Murgwanza wanahitaji  damu na huduma nyingine kama chakula na fedha za matibabu baada ya kutelekezwa na ndugu zao wakisubiria huruma na uzalendo wa wauguzi na madaktari wa hospitali hiyo

Mmoja wa wagonjwa waliotelekezwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Nyabisindu  wilayani Ngara na mkazi wa kijiji cha Djululigwa Revelian Wilson mwenye umri wa miaka 16  anayesumbuliwa na maradhi ya mguu ambapo  mahitaji makubwa ni dawa na chakula
Wanafunzi  vijana wa vyuo vikuu wanaotokea wilayani Ngara wamejitokeza kuchangia damu huku wakihimiza wananchi wengine kuonesha moyo wa huruma wa kujali wenzao kujitokeza kunusuru nguvu kazi ya taifa  ambapo wametoa msaada wa vinywaji na sabuni kwa wagonjwa
 
Kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Murugwanza Dkt Christian Ruzige amesema Hospitali hiyo yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 200 inahitaji chupa 30 mpaka 60 kila  mwezi kusaidia wagonjwa wenye mahitaji ya huduma hiyo.

Post a Comment

0 Comments