habari Mpya


Bukoba Senene kuuzwa shilingi 6000 hadi 12,000 kwa kila kilo moja.

Bukoba. Na Shaaban Ndyamukama Rk
Wajasiriamali wanawake  katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameanza kunufauika na msimu wa kupatikana kwa senene  ambao wanawauza kilo moja ambayo haijakaangwa Sh6000 huku kilo hiyo iki kaangwa na kuwekewa viungo inauzwa Sh12,000  kwa wateja wanaotoka ndani na nje ya manispaa hiyo.


Wakiongea na Radio Kwizera katika Mtaa wa Kashabo wajasiriamali hao wamesema senene hao wanapatikana mara mbili kwa mwaka kati ya Machi na April pamoja na Novemba hadi Desemba ambapo hupatikana kwa kunaswa na mwanga wa umeme tofauti na zamani walitua na kusafiri kwa mbalamwezi.

Aidha baadhi ya wanawake na watoto wa shule za msingi wanafanya shughuli ya  kumenya Senene hao kwa kuwaondoa mabawa  na miguu  kwa kilo moja hulipiwa Sh.1000 na mtu mmoja anauwezo wa kumenya kati ya kilo tano adi kilo saba kwa siku.

Wajasiriamali hao wanafanyia shughuli yao katika mtaa wa Kanoni darajani barabara kuu ya kuingia Stendi ambapo halmashauri ya manispaa ya Bukoba imewatengea eneo hilo  huku wakitakiwa kila mjasiriamali anayeuza Senene kulipa ushuru wa Sh.1000 kwa ajili ya usafi wa mazingira.

Malengo ya wajasiriamali hao ni kutafuta fedha za kujikwamua katika mahitaji ya familia lakinini wanafunzi wanapata fedha za kuongeza kipato kwa wazazi wao na kupata mahitaji ya vifaa vya kujifunzia wanapokuwa shuleni. 

Post a Comment

0 Comments