habari Mpya


Timu ya Financial fc yashindwa kutamba mbele ya Benaco fc yakubali kipigo cha goli 2-1.

Vikosi viwili ambavyo ni timu ya Financial fc walio vaa jezi nyekundu na Benaco fc walio vaa jezi za bluu zote timu za wilayani Ngara mkoani Kagera.
 
Financial imekubali kupoteza mchezo wake dhidi ya Benaco kwa kukubali kufungwa magoli 2-1katika mchezo ambao umepigwa jana Octoba 07,2018.
Mchezo huo ulio anza majira ya saa kumi na nusu katika uwanja wa Kemikimba mjini Benaco, Financial ndio walikuwa wakwanza kupata bao la kuongoza dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Frank.
Kikosi cha timu ya Financial fc wakiwa katika picha ya pamoja.
 
Hatahivyo bao hilo halikudum ambapo Benaco waliamka na kulisakama lango la Financial na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha Dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza baada ya kutokea papatupapatu za piga ni kupige katika lango la timu ya Financial fc.
Hadi timu hizo zina kwenda mapumziko zote zilitoka nje kwa kutoshana nguvu si Financial fc wa Benaco fc.
Pichani juu ni timu ya Bbenaco fc wakiwa katika picha ya pamoja.
 Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi huku Benaco wakionekana kushambulia kwa nguvu na hivyo kufanikiwa kufunga bao la pili na lakuongoza.
Mpaka mwamuzi anapuliza kipyenga cha kumaliza mpira Benaco fc iliibuka na ushindi wa goli 2-1dhidi ya Fgainancial fc.

Pichani juu wachezaji wa Timu ya Financial fc wakifanya mazoezi kabla ya mechi kuanza.
Pichani juu wakanza kutoka kulia ni mchezaji wa Timu ya Financial fc Laurent Gervas wapili ni Oscar na watatu ni Frank.
Pichani juu ni kikosi cha timu ya Financial fc

Post a Comment

0 Comments