habari Mpya


Mbunge Sengerema William Ngeleja alazimika kuzima moto na wananchi uliozuka katika eneo la mkutano.

Mbunge wa jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Bw.William Mganga Ngeleja amelazimika kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Sogoso kata ya Sima baada ya moto kushika na kuteketeza kichaka kilichokuwa karibu na eneo lilipangwa kwaajili ya mkutano wa kijiji.

Akiwasili katika eneo hilo kwenye mwendelezo wa ziara za kikazi jimboni humo Bw.Ngeleja ameshuhudia moto mkubwa ukiunguza kichaka huku wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo kwaajili ya mkutano wakipambana kuzima moto huo ambao unadaiwa kutokana na kuni za akina mama waliokuwa wakiandaa chakula kwaajili ya wananchi walio hudhuria katika mkutano huo {Nzengo}.

Mbunge wajimbo hilo akiambatana na msafara wake uliojumuisha viongozi wa CCM wilaya na wandishi wa  Habari kwa lengo la kusikiliza kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili wananchi.

Mmoja wa akina mama hao Bi.Elizabeth Jolam ameiambia Radio kwizera kuwa wakati wanaandaa chakula kwaajili ya Ugeni wa kijiji Chao moto umeruka na kushika majani na kusambaa haraka katika eneo kubwa kutokana na Jua kali hali iliyowapa wakati mgumu kuudhibiti na kupelekea wananchi wote waliohudhuria mkutanoni kuhamia kwenye shughuli ya kuzima moto huo.

Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Sengerema ameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho hasa katika shughuli za maendeleo.

Amesema kwakuwa wananchi hao naonesha juhudi za  kuamua kuanzisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwaajili ya watoto wa darasa la awali  ambao hulazimika kutembea zaid ya masaa 2 kwenda shule ya kijiji jirani cha Tunyenye na kwamba ofisi ya mbunge kupitia mfuko wa jimbo itachangia mabati 100 na mifuko ya saruji 40.

Post a Comment

0 Comments