habari Mpya


IFAHAMU SIRI YA USHINDI WA TUZO YA HABARI ZA MAJI TANZANIA ILIYOCHUKULIWA NA AMINA SEMAGOGWA.

Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera FM Amina Deogratius Semagogwa ameshinda tuzo ya Umahiri wa habari za maji nchini Tanzania.


Shirika la Shahidi wa Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Tanzania kupitia programuya Uhakika wa Maji inayofanyakazi ya  kubadilisha namna ambavyo rasilimali maji inasimamiwa kwa manufaa ya Watanzania wote, mazingira na kukua kwa uchumi wa Tanzania  mwezi Juni 2017 kupitika kwa  Mwenyekiti wa Bodi, Mhandisi Herbert Kashililah alizindua shindano la mwaka la Mwandishi Bora wa habari kuhusu uwajibikaji kwenye masuala ya maji, lijulikanalo kama “TUZO YA HABARI ZA MAJI”.

Lengo ikiwa ni Kutambua na kuthamini mchango muhimu wa waandishi wa habari katika kuelimisha na kupelekea utatuzi wa changamoto za usimamizi wa rasilimali maji nchini na Kuongeza uelewa wa vyombo vya habari na jamii kuhusu masuala ya maji.
Katika shindano hilo lililo washirikisha waandishi wa habari  120 kutoka katika  

vyombo mbalimbali vya habari kama magazeti, majarida, redio au tovuti na blogu zitakazohusu masuala ambayo wananchiwanakabiliana nayo kuhusu maswala ya uhakika na usalama wa maji.
Amina Deogratius Semagogwa wa Radio kwizera FM  ameibuka mshindi wa kwanza baada ya makala yake aliyotengeneza kukidhi vigezo na kuingia kwenye
Shindano hilo lilikuwa na  makundi  manne ambapo kundi la kwanza  ilikuwa ni Mwandishi Bora wa habari aliyetumia taarifa za Mradi wa Uhakika wa Maji,
kundi la pili  Uandishi bora wa kiasili kwa Uhakika wa Maji na kundi la tatu Mwandishi Bora wa habari za maji mwenye umri mdogo huku ikifatiwa na kundi la nne ambalo ilikuwa ni  Chombo Bora cha habari kuripoti kuhusu masuala ya maji.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam nakuhudhuriwa na waziri wa habari,Utamaduni,sanaa na michezo Dakt.Harrison Mwakyembe, Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso, Katibu mkuu wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo pamoja na wageni waalikwa kutoka sehem mbalimbali.
 
Ushindi huo ameupata baada ya kutengeneza makala ya   Sauti ya jamii iliyoangazia mradi wa maji kata ta Muhange Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma uliofadhiliwa na Benk ya Dunia kwa jumla ya shilingi millioni 720 tangu mwaka 2012 lengo ikiwa ukamilike baada ya miezi sita

Lakini hadi mwaka 2018 mwezi wa pili mradi huo ulikuwa haujakamilika ambapo baada ya makala hiyo ya sauti ya jamii kutupia jicho huko mpaka sasa baadhi ya maeneo ya kata ya muhange wananchi wake wameanza kupata maji huku maeneo yaliyobaki wakiendelea na matengenezo ili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo ya maji.

Post a Comment

0 Comments