habari Mpya


AMINA MTANGAZAJI WA RADIOKWIZERA FM ATWAA TUZO YA UANDISHI MAHIRI WA HABARI ZA MAJI

Pichani nimshindi wa habari za tuzo za habari za Maji AMINA SEMAGOGWA akikabidhiwa tuzo hiyo na waziri wa habari utamaduni, sanaa na michezo Dakt.Harrison Mwakyembe.
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa kipindi cha Mseto leo Radio kwizera fm Amina Semagogwa amepata tuzo ya umahiri wa uandishi wa habari za maji.

Tuzo hiyo ameipata baada ya kuibua tatizo la maji katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko mkoani Kigoma.  


Pichani wa kwanzakutoka kulia ni Mshindi wa Tuzo za umahiri wa habari za Maji akikabidhiwa  ngao na waziri wa habari ,utamaduni sanaa na michezo Dakt.Harrison Mwakyembe tuzo ambazo zimetolewa jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.
Post a Comment

0 Comments