habari Mpya


Yanga SC haoo Kileleni Ligi Kuu,Simba SC kuwaondoa dhidi ya Mbao FC leo ?

Yanga SC wamecheza na Coastal Union mechi ya Ligi kuu Tanzania bara 2018/2019 wakiwa nyumbani ,September 19,2018 wamefanikiwa kupata ushindi wa tatu mfululizo kwa kuifunga Coastal Union kwa goli 1-0, goli la Yanga SC likifungwa na Herietier Makambo dakika 11 kwa kutumia vyema pasi ya Ajib.

Ushindi huo sasa unaifanya Yanga SC kufikisha jumla ya point 9 na sasa wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao tu, kwani kwa pointi wanalingana na JKT Tanzania ilityocheza mechi 5, wote wakifuatiwa na Azam FC yenye point 8 za mechi nne na Simba SC, mabingwa watetezi wenye pointi 7 ambao leo September 20,2018 watacheza mechi yao ya nne dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza.

hapa chini ni matokeo ya michezo sita zilizochezwa Jumatano ya September 19 2018.

Post a Comment

0 Comments