habari Mpya


Wanakijiji Kakonko Waungana Kujenga Zahanati na Shule.

Na Faraja Marco –RK Kakonko.


Wananchi wa Kijiji cha Nyamwilonge, Kata ya Nyamtukuza wilayani Kakonko mkoani Kigoma  wakimsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Hosea Ndagalla  alipofika kwa lengo la kiwasikiliza kero zao.

 Katika mkutano huo wahadhara uliofanyika kijijini humo September 4, 2018 Wananchi wa Kijiji hicho cha Nyamwilonge, wamebainisha kuwa hulazimika kutembea zaidi ya kilomita 18 kutafuta  huduma ya matibabu nje ya kijiji chao.

Hata hivyo kijiji hicho licha ya kuwa na wakaazi zaidi ya elfu tano tangu mwaka 2002 hawana shule ambapo watoto hulazimika kutumia majengo ya makanisa Kujifunza Kusoma,Kuandika Na Kuhesabu  kwa kutumia walimu wa kujitolea.


Kutatua changamoto hizo, Wananchi  hao wa Kijiji cha Nyamwilonge, Kata ya Nyamtukuza wilayani Kakonko mkoani Kigoma  wamemuomba Mkuu wa wilaya ,Kanali Hosea Ndagalla  kusaidia Jitihada zao ambazo wameanza kukusanya mawe,kokoto na mchanga na wametenga eneo la kuanza ujenzi wa Zahanati na Shule kufikia mwishoni wa mwezi huu wa 9 kwa nguvu zao.

Post a Comment

0 Comments